Pages

Tuesday, December 8, 2015

"Mashabiki Msitushindanishe Wasanii, Mnatukosanisha" Vanessa Mdee

Mwanadada anayefanya vizuri na kibao, 'Never Ever', Vanessa Mdee amewataka mashabiki kuacha tabia ya kuwashindanisha wasanii au kuwagandamiza ili mmoja wao aonekane yupo juu.

Akizungumza katika kipindi cha Planet Bongo cha EATV jana, Vanessa alisema kila msanii ana nafasi yake katika muziki ndio maana ni vigumu kuwalinganisha. "Kuna baadhi ya mashabiki siyo wote, wenye tabia ya kugandamiza wasanii.

Tabia ya kupambanisha wasanii kwa sababu wana kitu fulani au ambao wanafanya kitu similar hii siyo hali nzuri," alisema Vanessa. Aliongeza, "Game ni ngumu kama mnavyoona, sasa tukianza kujadiliana sijui fulani ni fulani tunaweka ugumu kwenye lengo letu la kutengeneza muziki mzuri na kuleta burudani.

Kwahiyo mimi nampenda Shaa. Shaa ni mwanamke ambaye amekuwa kwenye game kwa miaka 10, amefanya kazi kubwa sana," alisema Vanessa. Kauli hiyo ya Vanessa imekuja kipindi kifupi baada ya Shaa kuulizwa anajisiaje pale mashabiki wanapomshindanisha na Vanessa.

"Niwambie ukweli sipendi sana hii tabia ya watanzania kunishindanisha na Vanessa Mdee au kitendo cha kuwashindanisha wasanii wa nyumbani, Shaa aliiambia Planet Bongo ya EATV.

"Huwezi kuwashindanisha watu ambao wapo kwenye boti moja, Mimi Shaa pamoja na Vanessa Mdee wote tunapeperusha bendera moja ya Tanzania hivyo unapotupambanisha ili iwe nini, ni bora hata ungenipambanisha na msanii kama Yemi Alade sababu yule ni msanii kutoka nchi nyingine" aliongeza Shaa.

Bongo 5

Source

No comments:

Post a Comment