![]() | ||
| Manager uhusiano wa Airtel bw Jakson Mmbando akiongea na waandishi wa habari |
![]() |
| Manager masoko bi Anethy Muga akitangaza majina ya top 5 |
![]() |
| All the best tano bora |
Airtel yatangaza tano bora ya shindano la Airtel Trace Music Stars
* Mshindi wa Airtel Trace Music kupatikana katika Finali
itakayofanyika tarehe 7 februari
Kampuni ya simu ya mkononi leo imetangaza washiriki walioingia tano bora
katika shindano la Airtel Trace Music star shindano lenye lengo la kusaka na
kuibua vibaji kwa wanamuziki chipukizi
Shindano hilo lililozinduliwa rasmi mwaka jana Oktaba limefika katika hatua
za fainali ambapo mshindi wa Airtel Trace T anzania atapatikana katika finali
inayotegemea kufanyika mwanzoni mwa mwenzi wa pili mwaka huu ambapo mshindi
huyu ataenda kushiriki mashindano ya Airtel Trace Music Stars Afrika
yatakayoshirikisha washiriki wengine kutoka nchi 13 barani Afrika
Akiongea na waandishi wa habari Meneja Masoko wa Airtel Bi Aneth Muga
alisema" leo tunayofuraha kubwa kutangaza majina ya washiriki waliofanya
vizuri katika mashindano haya na kupata nafasi ya kuingia katika tano bora
na kuweza kumpata mmoja kati yao atakaeibuka na ushindi wa kuiwakilisha nchi
yetu katika mashindano ya Airtel Trace Afrika".
Akiendelea kufafanua Aneth alisema "Washiriki hawa watano ni kati ya wengi
waliothubutu kuonyesha uwezo wao wa kushiriki kwa kupiga simu, kuimba na
kutuma nyimbo zao na hatimae majaji wamesikiliza vipaji vyao kama
walivyoimba na kuwachagua kuingia tano bora (top 5), sasa kura nyingi toka
kwa watanzania ndio itakayomuwezesha mmoja wao kupata uhindi wa kwanza wa
Airtel Trace Tanzania.
Mashindano haya yanalengo la kuinua vibaji vya musiki kwa vijana wetu
kuzifikia ndoto zao na kuwawezesha kuonyesha vipaji vyao ndani na nje ya
nchi. Airtel tunajisikia furaha kuwa sehemu ya mafanikio yao na sehemu ya
kuinua vipaji vya wanamuziki chipukizi kwa kupitia mashindano haya ya Airtel
Trace Music Stars. Napenda kuwapongeza na kuwatia hamasa wale wote
walioshiriki na pia hawa waliofanya vizuri na kufika katika hatua hii muhimu
ya mashindano haya.
Akitangaza majina ya walioibuka kwenye tano bora Meneja Uhusiano wa Airtel
Bw, Jackson Mmbando alisema " tunawashukuru watanzania na wanamuziki
chipukizi kwa kushiriki katika shindano hili na mpaka sasa tunaovijana wengi
waliojaribu kuonyesha uwezo wao wa kuimba, lakini kama mnavyofahamu haya ni
mashindao hivyo napenda kuwaleta kwenu wale waliofanya vizuri zaidi na
kuingia katika hatua hii ya mchuano mkali . waliobahatika kuingia tano bora
ni pamoja na Nalimi Mayunga mwenye namba ya ushiriki (YUN), Christopher
Kihwele (TOJ), Tracy Eminence (MHR), Beautus Henry (BOB) na Rose Mbuya (ROS)
Natoa wito kwa watanzania , wadau mbalimbali na wapenzi wa muziki kuwapigia
kura washiriki hawa kwa kupiga kutuma sms yenye jina la fumbo la mshiriki
kwenda kwenye namba 15594
Hii ni nafasi ya pekee kwa watanzania kuonyesha uwezo na vipaji vyao katika
anga za Afrika hivyo ni matumaini yetu kuwa washiriki hawa watajifua vyema
ili kufanya vizuri katika mashindano ya Afrika pindi mshindi atakapo
patikana.
Akiongea mara baada ya kutangaza kuwa moja ya tano bora Christophe r Kiwhele
alisema" najisikia furaha sana kupata nafasi hii ya kuwa moja ya tano bora,
kwakweli kwangu ni kama ndoto, siamini kama nimeweza kufudhu ma kufika
katika hatua hii kubwa, na amini ntaendelea kufanya vizuri kwani naendelea
kujiandaa vyema, nimetamani sana kuwa mwimbaji nyota na mwimbaji
anayenivutia zaidi ni Ed sheeran naamini kupitia mashindano haya ntafika
mbali na kutumiza ndoto zangu. Nawaomba watanzania watuunge mkono na
kutupigia kura ili kuendelea kufanya vizuri na hatimae kuwakilisha nchi yetu
vyema katika mashindano ya Afrika.
Washiriki tano bora wa Airtel Trace music Star sasa wako kambini ambapo
wanapata mafunzo yatakayoendelea hadi fainali inayotegeme kufanyika tarehe 7
mwenzi wa pili 2015 jijini Dar es saalam



No comments:
Post a Comment