Pages

Wednesday, January 14, 2015

TUESDAY SPECIAL.......

Heri ya mwaka mpya wadau wa Sintah blog,mie binafsi napenda sana kuwashukuru wale wote wanaotembelea blog hii,wawe wapenzi hata haters pia wanatupa changamoto kwa maneno yao,bila wao pia kijiwe hakinogi nawapenda wote.

Naomba Sintah topic ya leo mie niwaombe wale wajasiriamali wanaofanya biashara za kusafiri watupe uzoefu,haswa haswa nje ya nchi,ni vipi wanaweza kusafirisha mizigo wakishanunua,nina maana custom,mambo ya ushuru na kadhalika.Pili,nimepata kamtaji kama 5m,nataka nifanye biashara  nimeambiwa handbags zinalipa nchi za kusini, endapo nitapata soko,na kama nitapata kwa bei nzuri,naomba mnisaidie wale wazoefu wapi ambapo nitapata kwa bei ya jumla?na zaidi ya Handbags kipi ambacho naweza uza nikapata japo faida kidogo. 


Mwisho kuna wadau kama Vicky Lingerie,Tontoo na wengine,hawa waliwahi kutoa maushauri kibao mazuri sana, na hawakua wachoyo wa maujuzi, kwa faida ya wengine ambao hawakuwahi kusoma ile post,it was worth reading, if possible si vibaya wakatiririka tena tubadili upepo kidogo,tujijaze mapesa mifukoni (in mzee Cheyo's voice) hebu tusaidiane wanawake wenzangu,wanawake  ni jeshi kubwa tukitaka tunaweza,zile out of topic basi leo tuziache kwani ninaimani sote tutafaidika,Chonde msinipapure,kama huna cha kuchangia piga kimya usiharibu mood zetu wenye uchungu na maisha,twataka nasi tutoke kama wengine,hakuna hela yenye raha kama ya kuihangaikia mwenyewe




No comments:

Post a Comment