Pages

Tuesday, December 2, 2014

WEEKEND LIFE STORY

Leo naomba tubadilishe upepo wa wikiendi jamani,tuwepo kikazi zaidi,leo mimi naomba tupeane mbinu na namna gani tutaweza kujikwamua kiuchumi na kuacha kutegemea wanaume kama vyanzo vya kutuingizia kipato,japo sio wote tunategemea wanaume,lakini ni kweli wapo,hawajigusi kwa lolot,na bado wanataka kujirusha na kuwa na maisha fulani ambayo hawayamudu.Nnajua wengi humu ni waajiriwa,lakini si vibaya tukajiingiza pia katika ujasiriamali.

nilikuwa naomba kama ambavyo tunakuwa na OOT day,leo iwe ni Ujasiriamali day,nakumbuka katika post za nyuma kuna wadau humu walikua wanaulizia sana kuhusu topic hii,angalau topic za mapenzi tupumzike nazo,kwani mapenzi nayo kama pochi yako haisomi nayo ni majanga,hela ya kutafuta mwenyewe ina utamu wake na pia ni security fulani kwako wewe mwenyewe,sasa basi wadauz,tushauriane ni biashara,,project gani mtu waweza fanya,si lazima iwe ni biashara tu,kuna pia wenzetu ambao wanajua kuandika proposal za kuombea pesa,pia tujuzane,kuna ambao walikuwa wana mitaji,lakini hawajui nini wafanye,nafikiri hapa tuko mchanganyiko,hata kama ni mradi unaohitaji mtaji wa chini ya laki 5 tuambizane,kizuri tule wote,tumekua siku zote tunasaidiana kutatua matatizo,leo basi tusaidiane kujazana mahela.
NB:Wapendwa nawaombeni tu base kwenye ujasiriamali tu kwa leo,zile OOT ambazo hazihusu ujasiriamali hazitarushwa.




No comments:

Post a Comment